Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ng'ombe 200 wakamatwa ndani ya Bonde la Ihefu

18b335ccac7244f65a6bda7ab538ebc5 Ng'ombe 200 wakamatwa ndani ya Bonde la Ihefu

Wed, 27 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Zaidi ya ng'ombe 200 wamekamatwa ndani ya Bonde oevu la Ihefu, wilayani Mbarali, Mbeya katika operesheni ya kuondoa mifugo katika eneo lililopo ndani ya Hifadhi ya Ruaha.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kuagiza mifugo kuondolewa katika eneo hilo ndani ya siku sita.

Akizungumzia operesheni hiyo, leo , Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema kuwa uharibifu katika Bonde hilo utaathiri mtiririko wa maji katika Mto Ruaha.

Ameongeza kuwa eneo hilo linachangia asilimia 15 ya maji katika bwawa kuzalisha umeme la Nyerere ambalo bado lipo katika hatua ya ujenzi.

“Nipende kuwaasa wafugaji kiburi na ukaidi sio jambo zuri sana na wasije kuonesha kwamba kuna watu wapo nyuma yao sisi uwa hatuogopi watu bali tunafanya kutokana na taratibu na sheria zilizopo,” amesema Chalamila.

Aidha, Chalamila amekipongeza Chama cha Wafugaji nchini na hususani wilayani Mbarali kwa kushirikiana na Serikali katika kutoa elimu kwa wadau wake baada ya agizo la siku sita.

Chanzo: habarileo.co.tz