Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nesi auawa kwa kuchomwa kisu na mgonjwa aliyekuwa akimtibu

C2efce53 Acce 47f9 896d F9d6561ba7c5 Nesi auawa kwa kuchomwa kisu na mgonjwa aliyekuwa akimtibu

Sun, 23 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ripoti zinasema mgonjwa huyo alijihami kwa kisu na kumdunga nesi mara kadhaa hadi akafariki dunia.

June Onkundi alikuwa akimhudumia James Gomes mwenye miaka 47 wakati alichukua kisu na kumdunga mara kadhaa.

Kisa hicho kilifanyika katika hospitali ya Freedom House Recovery Centre saa saba mchana huku ripoti zikiibuka Gomes alikuwa na matatizo ya kiakili.

Onkundi ambaye ni kutoka kaunti ya Kisii, Kenya, alikimbizwa kwa matibabu lakini akafariki dunia alipokuwa akishughulikiwa.

Muungano wa manesi kutoka eneo la North Carolina (NCNA) kupitia kwa mkubwa wao Meka Ingram lilisema ni hofu kubwa kwamba Onkundi alifariki akiwahudumia wagonjwa.

Ametajwa kama mama na mke ambaye alikuwa amejitolea kuhakikisha kuwa anahudumia walio na matatizo ya kiakili.

Kisa hicho kilizua hofu kubwa miongoni mwa wahudumu wakihoji ni vipi usalama wao utapigwa jeki wanapowahudumia wagonjwa.

Gomes ametajwa kama mshukiwa ambaye amekuwa na visa vya kihalifu na amekuwa akifungwa jela mara kadhaa.

Katika mojawapo wa kisa cha awali, alikuwa ameshtakiwa kwa kujaribu kumbaka mfanyakazi mwenzake wakiwa kazini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live