Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nesi adaiwa kunaswa na kilo 174.77 za heroine Tabata

Madawa Ya Kulevya Muuguzi anaswa na pakti 162 dawa za kulevya

Fri, 3 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) inamshikilia Salum Mpangula ambaye ni muuguzi msaidizi katika zahanati iliyopo Kariakoo jijini Dar es Salaam kwa madai ya kukutwa na kilo 174.77 ya dawa za kulevya.

Mpangula alikamatwa na dawa hizo Mei 12 nyumbani kwake Tabata relini jijini Dar es Salaam zikiwa zimefungwa kwenye pakti 162.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 3, 2022 jijini hapa Kamishna Jenerali wa DCEA, Gerald Kusaya amesema mtuhumiwa huyo alinaswa akiwa na dawa hizo nyumbani kwake na alipohojiwa alidai kuwa ni mbolea.

“Dawa hizi zilikutwa zimewekwa kitandani halafu yeye mwenyewe amelala chini, alipoulizwa alisema ni mbolea lakini uchunguzi ulipofanyika ilithibitika kuwa ni heroin.

“Hadi sasa tunamshikilia tukiendelea na uchunguzi kubaini kama kuna wengine wanahusika katika uhalifu huu ili hatua zichukuliwe dhidi yao,” amesema Kusaya.

Kamishna Jenerali Kusaya ametumia fusra hiyo kuwatahadharisha watu wanaofanya biashara ya dawa za kulevya akiweka wazi kuwa mkono wa Serikali ni mrefu na utawafikia.

Advertisement “Kama kuna mtu anafikiria kutajirika kupitia biashara hii namshauri atafute shughuli nyingine, tumedhamiria kupambana na hakuna mtu anayeweza kuukwepa mkono wa Serikali tutamnasa tu,” amesema Kamisha Jenerali Kusaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live