Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndungulile: Tumekamata genge la wahalifu 17 wa mitandaoni

Bd5db95876979b2f8f3457adfff1c866 Ndungulile: Tumekamata genge la wahalifu 17 wa mitandaoni

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile amesema wizara yake imekamata genge la watu 17 waliokuwa wakifanya uhalifu mitandaoni waliokuwa wamejificha mkoani Morogoro.

Pia amesema wizara yake imeanza kampeni ya kushughulikia matapeli wa mitandano na wale wanaotumia lugha za matusi na kukashifu. Amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha mitandao inakuwa eneo salama kwa watu kufanya shughuli zao.

“Serikali imeanzisha kampeni ya kushughulika na watu wanaotoa lugha za matusi, kashfa na utapeli mitandaoni, hivyo wanaojihusisha na uhalifu huo waache mara moja kwani katika dunia ya Tehama huwezi kujificha.

“Kazi imeanza, tumekamata genge la watu 17 waliokuwa wakifanya uhalifu mitandaoni waliokuwa wamejificha mkoani Morogoro na muda wowote watafikishwa mahakamani,”alisema.

Dk Ndugulile amewataka Watanzania wanaotumia mitandao, kukosoa viongozi kwa hoja na lugha za staha na kuwa lugha za matusi, kashfa na kejeli, hazitavumiliwa.

“Kukosoa serikali na viongozi ni haki ya Mtanzania, lakini si kukosoa kwa lugha za matusi, kejeli na kashfa. Watu wa namna hii hatutawavumilia. Hakutakuwa na msalie mtume na mtu anayekwenda kinyume na taratibu na sheria za nchi. Tunawaeleza kuwa wasije kulaumu mtu tutakapoanza kuchukua hatua,”alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz