Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugu wasusa mwili anayedaiwa kufa kwa kipigo cha polisi Dodoma

Mon, 13 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mwili wa Hilary Shirima (19) leo Mei 11 umefikisha siku ya 10 tangu ndugu zake waususe katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma wakitaka kufanyika kwa uchunguzi juu ya kifo chake.

Shirima alifikishwa hospitalini hapo Aprili 29 hali yake ikiwa mbaya kwa kile kinachodaiwa ni kutokana na kipigo cha polisi.

Baba mdogo wa marehemu, Zubery Joseph jana aliliambia Mwananchi kuwa, ndugu yao alifariki dunia usiku wa kuamkia Mei 2 katika hospitali hiyo kutokana na majeraha aliyodai kuyapata kutokana na kupigo cha polisi.

“Hatuta uchukua mwili wa ndugu yetu kwasababu tunajua alikufa kwa kipigo cha polisi wakishirikiana na aliyekuwa mwajiri wake,” alisema.

Joseph alisema majirani walieleza kuwa, Aprili 28 mwaka huu walimsikia Shirima akipiga mayowe kuomba msaada na kwamba walipoenda walikuta akipigwa na tajiri yake kwa .tuhuma ya kusababisha hasara katika duka alilokuwa anauza.

“Hata hivyo, tumezungushwa sana polisi, yaani bila kujiongeza hadi kwa Kamanda (Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gilles Muroto) huenda hata mwili wa ndugu yetu ingekuwa ni shida kuupata, katika hili namshukuru Muroto amesimama katika nafasi yake,” alisema Joseph.

Pia Soma

Alisema mwili wa ndugu yao unaonekana hata kwa macho kuwa na alama za vipigo lakini polisi wanadai amekufa kwa kuzidiwa na dawa za kulevya.

Juzi Mwananchi lilifika katika hospitali hiyo, ambapo mmoja wa wagonjwa alikiri kijana huyo kupelekwa hospitalini akiwa hajitambui huku akiwa amefungwa pingu.

“Kweli nilimuona na mimi ndiye niliwambia ndugu yake yule kijana alikuja amefungwa pingu akawekwa dripu mbili lakini baada ya hali yake kuwa mbaya polisi alimfungua pingu na kumtelekeza,” alisema.

Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Kamanda Muroto alisema jambo hilo analifuatilia kwa karibu ili kuona kama kuna polisi amehusika na kifo hicho ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz