Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugu wa waliouawa kwa iamni za kishirikina waiangukia polisi, waomba ulinzi

Ndugu wa waliouawa kwa iamni za kishirikina waiangukia polisi, waomba ulinzi

Sun, 5 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kasulu. Siku chache baada ya watu wanne wa familia moja ya mganga wa kienyeji kuuawa  akiwamo mjamzito kwa kukatwa panga  na wananchi pamoja na kuchomewa mali na nyumba kubomolewa kwa tuhuma za kujihusisha na imani  za ushirikina,  ndugu  wameomba ulinzi kwa jeshi la polisi.

Tukio hilo lililotokea Januari 2, mwaka 2020, nyakati za usiku  katika Mtaa wa Katandala Kata ya Msambara,  Wilayani Kasulu mkoani Kigoma. 

Waliouawa ni Petro Sagalika ambaye ni mganga wa kienyeji , mkewe Suzana Mkuka, na watoto wao Fonsi na Aniza  Petro aliyekuwa mjamzito.

Mtoto mkubwa wa marehemu, Daud Sagalika alisema tukio hilo limeacha simanzi na kovu katika maisha yao baada ya wazazi na ndugu zao kuuawa kikatili na wananchi na kwamba wamekuwa wakiishi kwa hofu na kuiomba serikali iwape ulinzi.

Alisema kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi na kufanya ukatili huo usipochukuliwa hatua za haraka na serikali kwa wananchi waliohusika, matukio kama hayo yatajirudia tena.

“Wananchi wamefanya ukatili kwa familia yangu kesho wanaweza kufanya kwa familia nyingine, niiombe serikali iweze kuchukua kuhakikisha waliohusika na tukio hilo wanakamatwa na sisi tunaomba ulinzi kwani tumekuwa tukiishi kwa hofu,” amesema Sagalika.

Ndugu mwingine wa familia hiyo, Simon  Sagalika amesema  wakati wa tukio hilo wananchi walianza kujikusanya na kuvamia nyumbani kwa baba yake na kuanza kuwashambulia kwa kuwachukua na kuwakatakata mapanga.

Amesema pamoja na kufanya mauaji wamebomoa nyumba tatu za familia na kufyeka migomba na kwamba baada ya mauaji hayo polisi walichukua miili na kuifanyia uchunguzi na baadaye kuruhusu familia izike ambapo miili hiyo imezikwa katika kati ya nyumba za familia hiyo.

Diwani wa Msambara, Evansi Buchonko  amesema sababu kubwa ya mauaji hayo inatajwa kuwa imani za kishirikina.

Inadaiwa mzee wa familia hiyo alikuwa mganga wa kienyeji na alikuwa a akituhumiwa na wananchi wa mtaa huo na vijiji jirani kuhusika katika mauaji ya baadhi ya watu.

Amesema walilazimika kutoa taarifa  polisi usiku wa tukio ambapo polisi waifika na kukuta mauaji yalishafanywa ambapo marehemu wote walitolewa nje na kuuliwa barabarani nje ya nyumba yao huku baadhi ya wanafamilia wakifanikiwa kuokoka katika tukio hilo ambapo inasadikiwa pia baadhi ya watoto walijificha mashamabani.

Mkuu wa wilaya ya Kasulu, Kanali Simon Anange amesema vyombo vya dola vinafanya uchunguzi juu ya  tukio hilo huku akiwaonya wananchi  ambao wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi na kuwaua watuhumiwa na kwamba kufanya matukio kama hayo kwa Imani za kishirikina ni kosa.

Chanzo: mwananchi.co.tz