Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndugu, jamaa waruhusiwa mahakamani kesi ya kusafirisha shehena ya dhahabu

Wed, 22 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza.  Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza, Rhoda Ngimilanga amekubali hoja iliyotolewa na upande wa utetezi jana ukilalamikia polisi kuwazuia ndugu wa washtakiwa katika kesi ya kusafirisha shehena ya dhahabu kuingia ndani ya mahakama kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.

Kesi hiyo namba 1/2019 inawakabili waliokuwa askari wanane katika wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza ambao wanadaiwa kusafirisha kilo 319 ya dhahabu yenye thamani ya Sh27.18 bilioni.

Jana Jumanne Mei 21, 2019 wakili wa utetezi Deo Mgengeli aliomba mahakama iwaruhusu ndugu, jamaa, marafiki na watu wote wenye maslahi na kesi hiyo kuingia kufuatilia maana ni haki yao kama sheria ya mahakama ya wazi inavyoeleza.

"Mahakama imepokonywa mamlaka yake kuwazuia watu na ndugu za washatakiwa kuingia ndani."

Naye mkurugenzi wa makosa ya rushwa na utakatishaji fedha katika ofisi ya taifa ya DPP, Fredrick Manyanda alidai kwamba walizuia watu kutokana na sababu za kiusalama katika eneo hilo.

Akitoa uamuzi leo Mei 22, 2019 kabla ya kuanza kusikiliza shauri hilo,  Hakimu Ngimilanga amesema Mahakama haijazuia wananchi kuingia kusikiliza shauri hilo maana ni haki yao kisheria.

Pia Soma

Amesema suala la usalama ni jukumu la polisi hivyo wanatakiwa kuhakikisha usalama upo wakati wote shughuli za mahakama zikiendelea hivyo hakuna sababu ya kuwazuia watu kuingia ndani kusikiliza iwapo hakuna vitendo vya kuashiria uvunjifu wa amani

Chanzo: mwananchi.co.tz