Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nchi zingine zaongezwa kufanya upelelezi kesi ya Acacia

60705 PIC+ACCASIA

Fri, 31 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Upande wa mashtaka katika kesi inaowakabili vigogo wa Kampuni ya Acacia akiwamo aliyekua Makamu wa Raisi, Deo Mwanyika wameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kuna nchi nyingine zimeongezeka kwa ajili ya kufanya upelelezi.

Wakili wa Serikali Wankyo Saimo amedai leo Mei 31,2019 mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi bado haujakamilika.

"Kesi imekuja kwa ajili ya kutajwa upelelezi haujakamilika kwa sasa kuna nchi nyingine zimeongezeka kufanya upelelezi hivyo tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa" amedai Wakili Wankyo

Hata hivyo, wakili wa utetezi, Rweikama Rweikiza ameuomba upande wa Jamhuri kuharakisha upelelezi ili kesi hiyo iweze kuanza kusikilizwa.

Hata hivyo, Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo hadi Juni 14, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Meneja Uhusiano wa Mgodi wa Bulyanhulu Alex Lugendo,  Mkurugenzi mtendaji wa Pongea, North Mara na Bulyanhuku Assa Mwaipopo, Kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.

Pia Soma

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka 39, yakiwemo ya utakatishaji na kukwepa kodi zaidi ya fedha za Marekani milioni 112.

 

Washtakiwa hao pia wanakabiliwa na mashtaka matatu ya kula njama , mashtaka saba ya kughushi , mashitaka 17 ya Utakatishaji wa fedha, Kuwasilisha nyaraka  za uongo  kwa  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), shtaka moja, kuongoza uhalifu wa kupangwa, mashitaka nane ya kukwepa kodi na shitaka moja la kutoa rushwa.

Wanadaiwa, kutenda makosa hayo kati ya Aprili 11,  mwaka 2008 na Juni 30, mwaka 2007 katika sehemu tofauti ya jiji la Dar es Salaam, Kahama Mkoani Shinyanga, Tarime Mara, Biharamulo Kagera maeneo ambayo yapo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maeneo mengine ambayo washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo ni katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, Toronto Canada na nchini  Uingereza.

Aidha, mshtakiwa Mwanyika  na Lugendo, wanadaiwa kutoa msaada katika kusimamia mkakati wa kihalifu kwa nia ya kupata faida.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutoa tamko la uongo kwa Kamishna Generali wa TRA huko Biharamulo kwa nia ya kukwepa kulipa kodi ya dola za Marekani 9,309,600 ambayo ilikuwa ni kodi iliyopaswa kulipwa kwa TRA.

 

Mwanyika na Lugendo wanadaiwa kuwa kati ya Desemba mwaka  2009 na  Julai  31, mwaka  2018 katika maeneo tofauti ndani na nje ya nchi ya Tanzania kwa pamoja na wengine ambao hawapo mahakamani, walisaidia mgodi wa North Mara kuhamisha fedha kiasi cha dola  za Marekani 374,243,943,45 huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la makosa ya kughushi na kukwepa kodi.

Pia wanadaiwa kati ya Novemba 2, mwaka  2012 na Novemba 27,  mwaka 2015 huko Shinyanga walitoa rushwa ya sh. 718,520,001.76 kwa Hussein Kashindye ambaye  ni mkuu wa upelelezi makosa ya jinai wa Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kumshawishi ili aweze kuachana na uchunguzi wa makosa ya jinai yaliyokuwa yametendwa na Mgodi wa Bulyanhulu.

Chanzo: mwananchi.co.tz