Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Naomi ajinyonga kwa Kitenge na mtandio Katoro

Kifo Kifo Mauiaji.png Naomi ajinyonga kwa Kitenge na mtandio Katoro

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naomi Mahalu (34) mkazi wa Mtaa wa CCM, Kitongoji cha Lutozo Kata ya Katoro mkoani Geita, amekutwa amejinyonga ndani kwake kwa kutumia kitenge alichokiunganisha na mtandio huku sababu iliyopelekea mwanamke huyo kufanya tukio hilo haijajulikana.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema marehemu alikua ni mfanya biashara wa dagaa hivyo alikua na kawaida ya kutoka alfajiri kwenda kufanya usafi kwenye eneo lake la biashara kisha kurudi nyumbani lakini siku ya jana hakuonekana akitoka wala kurudi nyumbani kwake ndipo wakaingiwa na hofu iliyowapelekea waingie ndani kwake kuangalia nini kinaendelea.

Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya Katoro amethibitisha kupokea mwili wa marehemu na kusema wameuhifadhi kusubiri hatua za utambuzi kutoka kwa ndugu wa marehemu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live