Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzungu miaka 80 afungwa miezi 6 jkwa kuishi nchini bila kibali

Kikongwe Mzungu miaka 80 afungwa miezi 6 jela kwa kuishi nchini bila kibali

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Raia wa Ufaransa, Aboudou Mze (80) amehukumiwa kulipa faini ya Sh 500,000 au kwenda jela miezi sita, baada ya kupatikana na hatia ya kuishi nchini bila kuwa na kibali.

Mze amehukumiwa kifungo hicho leo Alhamisi Septemba 9, 2021 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya mshtakiwa kukiri shtaka lake.

Mbali na adhabu, mahakama hiyo imeamuru Idara ya Uhamiaji kumrudisha nchini kwao (Ufaransa) mshtakiwa huyo.

"Mahakama imekutia hatiani kama ulivyoshtakiwa hiyo, utatakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 na ukishindwa kulipa faini hii, basi utatumikia kifungo cha miezi sita jela," amesema Hakimu Simba.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo ameshindwa kulipa faini hiyo na hivyo atatumikia kifungo hicho jela.

Awali, Mwendesha Mashtaka kutoka Idara ya Uhamiaji, Shija Sitta ameiomba mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine, wanaokaa nchini bila kuwa kibali.

Akimsomea shtaka lake, Wakili Sitta alidai kuwa Mze anadaiwa kutenda kosa lake Septemba 6, 2021, katika Ofisi za Uhamiaji zilizopo Kurasini.

Siku hiyo, Mze akiwa raia wa Ufaransa alikutwa akiishi nchini bila kuwa kibali, wakati akijua kuwa ni kinyume cha sheria.

Chanzo: Mwananchi