Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee wa miaka 60 akiri kulawiti mtoto wa miaka 7, afungwa jela maisha

Mzee Pic Data Mzee wa miaka 60 akiri kulawiti mtoto wa miaka 7, afungwa jela maisha

Tue, 13 Sep 2022 Chanzo: Mwananchi

Mzee wa miaka 60, Dickson Njau au ‘Babuu Saluu’, mkazi wa KDC Mbokomu katika wilaya ya Moshi, amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukiri kosa la kumlawiti mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka saba.

Mshitakiwa ambaye hakuisumbua mahakama, alikiri kumwingiza mtoto huyo chumbani, kumvua nguo na kumpaka mafuta na kumwingizia uume wake, lakini haukuingia vizuri na kujitetea kuwa yote aliyoyafanya ni shetani alimwingilia.

Mzee huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi jana Septemba 12, 2022 na kusomewa mashitaka na maelezo ya kosa hilo na wakili mwandamizi wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashitaka (NPS), Kassim Nassir na kukiri kosa.

Akimsomea shitaka hilo mbele ya Hakimu Mkazi, Rehema Olambo, wakili Nassir , alieleza kuwa Septemba 7,2022 huko KDC Mbokomu, mshitakiwa alimwingilia mtoto huyo mwenye umri wa miaka 7 kinyume cha sheria za Nchi.

Hata hivyo mshitakiwa alikanusha shitaka hilo na upande wa mashitaka ukaomba kumsomea maelezo ya kosa lake, na hapo ndipo alipoyakubali na kusema kuwa ingawa alimpaka mafuta mtoto na kuingiza uume, lakini haukuingia ipasavyo.

Akimsomea maelezo hayo, wakili Nassir alisema siku ya tukio, mtoto huyo alienda kucheza nyumbani kwa mshitakiwa ambapo baadae mshitakiwa alimshika mkono na kumpeleka chumbani kwake na kumvua suruali aliyovaa na kumpaka mafuta.

Kulingana na maelezo hayo, mshitakiwa aliingiza uume wake kwa mtoto huyo ambaye alipata maumivu ndipo mshitakiwa akaacha kuendelea na kitendo hicho, ambapo mtoto huyo alirudi nyumbani kwao na kukutana na bibi yake.

Bibi yake huyo wakati anataka kumuogesha, alibaini mtoto huyo akiwa amepakwa mafuta matakoni na alipomuuliza ndipo akaeleza kila kitu alichofanyiwa na mshitakiwa ndipo mama mzazi alijulisha ba baadae mshitakiwa kutiwa mbaroni.

Baada ya kusomwa kwa maelezo hayo, mshitakiwa alikubaliana nayo yote isipokuwa akasema hakuwa amefikia hatua ya kumlawiti kwa kuwa uume wake haukuingia licha ya kumpaka mafuta mtoto huyo.

Kutokana na maelezo hayo, Hakimu Olambo alimweleza mshitakiwa kuwa kwa kuwa amekiri maelezo yaliyosomwa na kukiri kumpaka mtoto mafuta na kuingiza uume sehemu ya haja kubwa, hiyo inathibitisha alimwingilia mtoto huyo.

Baada ya kumtia hatiani, mshitakiwa aliomba apunguziwe adhabu kwani ana majukumu ya kumlea mama yake mzazi ambaye anaishi naye hivyo akifungwa hatakuwa na mtu wa kumwangalia na kwamba yeye anaumwa kifua na magoti.

Hakimu Olambo baada ya kusikiliza maungamo hayo, alisema sheria imemfunga mikono na kwamba adhabu ya kosa alilolitenda ni kifungo cha maisha jela.

Chanzo: Mwananchi