Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee wa miaka 50 mbaroni kubaka

Kulawiti Pc Data Mzee wa miaka 50 mbaroni kubaka

Sat, 25 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja mwenye umri zaidi ya miaka 50 aliyejulikana kwa jina la Hakimu Juma, mkazi wa Chamwenda kata ya Nyasaka wilayani Ilemela jijini Mwanza amejikuta matatani baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kumbaka binti wa miaka saba mtoto wa jirani yake.

Inadaiwa kwamba mzee huyo amekuwa na tabia ya kuwashika makalio pamoja na sehemu za siri mabinti wa mtaa huo hadi alipofikia hatua ya kumuingilia kimwili binti huyo wa miaka saba anayesoma darasa la pili

Mama mzazi wa binti aliyebakwa aaaakaeleza namna alivyogundua tukio hilo la binti yake kuingiliwa na baba huyo.

"Nilikuwa namwambia sasa wewe unaumwa hujasema umepatwa na nini, sasa nikawa namuangalia nikaona suruali aliyokuwa amevaa ipo magotini na chupi pia imevuliwa nikamgeuza wakati namgeuza nikaona michirizi kalowa nikauliza wewe umepata UTI niliponusa mashuka nikasikia harufu ya maji ya kiume"

Akizungunza nasi, Balozi wa serikali ya mtaa huo wa Chamwenda Hassan Ngiziki amesema mara baada ya mtuhumiwa huyo kufanya tukio hilo walibaini kuwa amekuwa na tabia ya kushika makalio na sehemu za siri baadhi ya mabinti wa mtaa huo ndipo akawasiliana na vyombo vya dola na kumkabidhi kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live