Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee akamatwa kwa kumiliki kiwanda cha kutengeneza silaha (+picha)

Screenshot 2021 02 03 At 09.45.53 660x400.png Mzee akamatwa kwa kumiliki kiwanda cha kutengeneza silaha (+picha)

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia, Shabani Athumani (61) mkazi wa Kwamakocho, Chalinze akituhumiwa kumiliki kiwanda cha kutengenezea silaha mbalimbali za moto.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio la kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo limetokea Januari  31, saa 1 jioni.

Kwa mujibu wa Nyigesa, kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulitokana na ushirikiano wa raia mwema na kwamba baada ya kupata taarifa hizo walifanya uchunguzi na kisha kubaini uwepo wa kiwanda hicho.

Amesema katika uchunguzi huo Jeshi la Polisi lilimkamata mtuhumiwa huyo akiwa na mtambo wa kufulia vyuma, chupa 5 ndogo zenye baruti ndani yake, Fataki 48 na risasi 42 za bunduki aina Gobole na  Paketi 1 ya unga wa Kiberiti.

Nyigesa ametaja vifaa vingine kuwa ni mitambo mitatu ya Silaha aina ya gobole ambayo ipo tayari bado kuwekwa mtutu na kitako, mitambo ya kutobolea vifaa vya miti vinavyotumika kwenye silaha aina gobole na kopo moja lenye unga wa tindikali ambalo unatumika kuunganisha vyuma vinavyofungwa kwenye silaha aina  ya gobole.

UKWELI WA MAISHA YA CHIKUMBALAGA, MAMA YAKE, MISIBA, HARUSI ZOTE ZAKE, HELA ANAYOINGIZA

Chanzo: millardayo.com