Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzee adakwa akisafirisha bangi JNIA

Bangijpg Pichaa Mzee adakwa akisafirisha bangi JNIA

Wed, 19 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam, kwa nyakati tofauti limewakamata watu sita kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya bangi zenye uzito wa jumla ya kilo 17.134 kwenda Dubai.

Miongoni mwa watu waliokamatwa ni Rashid Kumkana, ambaye ni mzee mwenye umri wa miaka 74.

Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege Tanzania, Mary Kipesha amesema, Kumkana amekamatwa jioni ya Aprili 17, 2023 katika jengo la tatu la abiria eneo la ukaguzi wa mwisho akiwa na dawa hizo za kulevya.

Amesema mtuhumiwa huyo alikuwa akisafiri kuelekea Dubai na ndege ya shirika la ndege la Fly Dubai kupitia Zanzibar, akiwa na begi moja la mgongoni.

Kamanda Kipesha amesema walipokagua ndani kwenye begi la Mzee Kumkana walikuta pakiti moja yenye dawa za kulevya aina ya bangi iliyoshonewa ndani ya begi, na zingine alifunga kitaalam kiunoni akiwa amevalia kanzu ambazo jumla zilikuwa kilo 3.66.

wengine waliokamatwa JNIA wakituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya ni Rehema Ally (42) na wengine ambao majina yao hayatajwa kutokana na upelelezi unaoendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live