Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzazi mbaroni kwa kutaka kumuozesha mwanaye

77419 Ndoa+pic

Fri, 27 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Amos Ryoba, mzazi wa mwanafunzi wa kidato cha tatu Shule ya Sekondari  Zogowales  mkoani Pwani amekamatwa na Jeshi la Polisi wilayani Ilala, Dar es Salaam kwa madai ya kutaka kumuozesha mwanaye mkoani Mara.

Alipoulizwa kuhusu jambo hilo, Ryoba anayeshikiliwa na polisi kituo cha Stakishari alikiri kutaka kumsafirisha mwanaye kwa madai kuwa ameshindwa kumlipia ada aishi bwenini.

“Mtoto mwenyewe mtukutu nikimwambia apike anakataa kazi yake ni kuchati tu  siku nilipochukua simu yake nitazame huwa anawasiliana na nani, alichukua nguo zangu na kuzichoma moto. Baada ya hapo nilikubaliana na ndugu zangu tumrejeshe kijijini ili akaolewe na mtu yeyote,” amesema Ryoba.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 16, amelieleza Mwananchi kuwa ana wiki tatu hajakwenda shule baada ya kuelezwa na Ryoba hawezi kumlipia Sh500,000 za bweni.

Amesema Septemba 23, 2019 alielezwa na baba yake kuwa anakwenda Ubungo kumkatia tiketi ya basi kwenda kijiji cha  Magoma Wilaya ya Tarime mkoani humo

“Alipoondoka nikaruka ukuta na kwenda kwa mama anayeishi Majohe kumueleza yaliyonipata na (mama) akaniambia hawezi kuishi na mimi kwa kuwa ni mwanafunzi natakiwa kuwa shule,” amesema.

Pia Soma

Advertisement
Mariam, ambaye ni mama wa mtoto huyo amesema alimpeleka mwanaye katika ofisi za Serikali ya mtaa na kushauriwa aende polisi.

“Ndio nikaja hapa Stakishari na kufungua jalada lenye namba STK/RB/9956/2019 ya kumkatisha masomo mwanafunzi kwa nia ya kumuozesha,” amesema Mariam.

Hadi Mwananchi linaondoka kituoni hapo leo saa 9 alasiri, mtuhumiwa huyo alikuwa bado anashikiliwa.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz