Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mzazi adai mwanae aliuawa

Pisi.jpeg Mzazi adai mwanae aliuawa

Sat, 8 Oct 2022 Chanzo: Eatv

Mama mzazi wa  binti aliyepoteza maisha kwenye maandamano nchini Iran, amezishutumu mamlaka za nchi hiyo kwa mauaji ya binti yake

Nasrin Shakarami mwenye umri wa miaka 16  alipoteza maisha kwenye maandamano hayo ambapo kwa mujibu wa mama yake mwili wake ulikutwa na majeraha huku taarifa ikitofautiana na ya polisi.

Mamlaka zinasema kwamba Nika Shakarami (16) huenda alirushwa kutoka kwenye jengo refu na mafundi wajenzi , ambapo alipotea tangu tarehe  20 mwezi uliopita baada ya kuwaeleza rafiki zake kwamba anakimbizwa na polisi. 

Mamlaka zinasema kwamba binti huyo alikutwa amepoteza maisha kwenye jengo aliloingia usiku ambapo mwili wake ulikutwa nje ya jengo nyakati za asubuhi.  

Kifo cha Nika Shakarami kinakua ni jeraha lingine kwa waaandamanaji nchini Iran ambao wanaandamana toka mwezi jana wakipinga kile wanachokiita mauaji ya mwanamke mwingine aitwae Mahsa Amini ambaye alipoteza maisha baada ya kukamatwa na askari kwa kosa la kutovaa hijabu.

Chanzo: Eatv