Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwizi aliyekosa fedha kanisani aacha barua ya kuomba radhi

66847 Pic+mwizi

Mon, 15 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Nairobi, Kenya. Unaweza kufikiria ni tamthilia lakini ni kweli imetokea nchini Kenya baada ya mtu anayesadikiwa kuwa mwizi kuvunja madhabau ya kanisa kwa lengo la kuiba kuacha barua ya kuomba radhi.

Mtu huyo alifanya tukio hilo usiku wa kuamkia Jumapili katika Kanisa la Pentekosti Nyandarua lililopo jijini Nairobi Kenya.

Inadaiwa kuwa mwizi huyo aliandika ujumbe huo bada ya kukosa fedha katika madhabau hayo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation la Kenya, tukio hilo litokea miezi michache baada ya uongozi kukamata watu watatu wanaosadikiwa kuhusika na wizi katika kanisa hilo.

Barua hiyo iliyosomwa kwa waumini wakati wa ibada ya Jumapili, mwizi huyo alisema anajutia kitendo alichofanya na kuomba asamehewe.

 “Nimeelekezwa na mmoja wa waumini ambaye aliniambia fedha zinahifadhiwa ndani ya kanisa, lakini nilipofika sikukuta kiasi chochote, Mungu awabariki na mniombee,” ilisema sehemu ya barua hiyo.

Pia Soma

Mchungaji wa kanisa hilo, Peter Wanyoike alidhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mwizi huyo aliingia ndani baada ya kukata sehemu ya bati.

“Tulikuta barua ndani ya kanisa wakati polisi walipofika kwa ajili ya upelelezi wa tukio hilo. Aliamini kuna kiasi kikubwa cha fedha ndan; tumemsamehe na tunamuombea aokoke. Tunamkaribisha aje kutubu na kusali pamoja nasi,” alisisitiza Mchunaji Wanyoike.

Chanzo: mwananchi.co.tz