Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwingine aunganishwa kesi ya uhujumu uchumi, wafikia 10

Picha Uhujumu Uchumi shatakiwa Godfrey Joseph akirudishwa mahabusu baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabil

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Mfanyabiashara wa madini ya dhahabu, Geodfrey Joseph mkazi wa Kahama mkoani Shinyanga ameunganishwa katika kesi ya uhujumu Uchumi na utakatishaji fedha iliyokuwa ikiwakabili wafanyabiashara wengine tisa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita.

Mwanasheria wa Serikali, Scolastica Teffe ameieleza mahakama leo Jumanne Julai 11, 2023 kuwa kesi hiyo imekuja kwa hati ya dharura baada ya kuongezeka kwa mshtakiwa wa 10 pamoja na kuongezeka kwa mashtaka dhidi ya mstakiwa wa kwanza na wanane hivyo kufanya mashtaka yanayowakabili kuongezeka kutoka 49 hadi 55.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Cleofas Waane Wakili wa Serikali, Scolastica Teffe akisoma mashtaka yanayomkabili mshtakiwa wa kumi amedai anashtakiwa kwa kosa la kufanya biashara ya madini bila kuwa na kibali kinyume na kifungu cha 18(1)4a ya sheria ya madini ya mwaka 2019 pamoja na aya ya 27 jedwali la 1 kifungu cha 57 (1&2) ya uhujumu Uchumi ya mwaka 2022.

Amedai mshatakiwa huyo kwa tarehe tofauti kati ya Januari mosi 2022 na Juni 31, 2023 ndani ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga alitoa gram 5,000 za dhahabu zenye thamani ya zaidi ya Sh725 milioni bila kuwa na kibali.

Shtaka jingine ni kuisababishia mamlaka hasara kinyue na aya ya 10(1) jedwali la 1 kifungu cha 57(1, 60 (2) cha sheria ya makosa ya uhujumu uchumi ya mwaka 2022.

Mshatakiwa huyo anadaiwa kwa tarehe tofauti kati ya Januari Mosi, 2022 na 30 Juni, 2023 ndani ya Wilaya ya Kahama kwa kuwa na nia ovu aliisababishia tume ya madini kupata hasara ya Sh43.5 milioni fedha ambazo zilipaswa kulipwa kama tozo ya mrabaha kwa Serikali.

Katika shtaka la 52 mshtakiwa huyo anadaiwa kuisababishia mamlaka hasara ambapo anadawa kati ya Januari Mosi na Juni 30, 2023 mshtakiwa huyo akiwa Kahama kwa nia ovu aliisababishia hasara ya Sh7.2 milioni tume ya madini iliyopaswa kulipwa kama ushuru wa ukaguzi.

Mshtakiwa huyo anashtakiwa kwa kuisababishia mamlaka hasara ambapo katika kipindi hicho hicho aliisababishia tume ya madini hasara ya Sh2.1 milioni fedha zilizopaswa kulipwa kama tozo ya ushuru wa huduma.

Chanzo: Mwananchi