Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwimbaji nyimbo za injili adaiwa kumuua mkewe kwa shoka

90064 Mauaji+pic Mwimbaji nyimbo za injili adaiwa kumuua mkewe kwa shoka

Sat, 28 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha/Serengeti. Polisi inamtafuta Moses Pallangyo akihusishwa na mauaji ya mkewe Mary Richard, mkazi wa kijiji cha Kilinga wilayani Arumeru, ambaye aliuawa kwa kukatwa na shoka.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shana alisema tukio hilo lilitokea juzi na linasadikiwa kuwa linatokana na ugomvi wa kifamilia.

“Baada ya kufanya mauaji, ametoroka na tunamsaka. Chanzo cha ugomvi hakijulikani, lakini taarifa za awali zinaeleza huenda ni wivu wa mapenzi,” alisema Shana.

Pallangyo, ambaye ni maarufu kwa jina la Moses Lebaba, ni mwimbaji wa nyimbo za injili mkoani Arusha. Baba wa mtuhumiwa, Latiaeli Pallangyo alisema tukio hilo limetokea ikiwa ni wiki tatu tangu Mary aanze kuishi na mwanae.

“Hapakuwapo na ugomvi wowote na walitegemea kusherehekea sikukuu ya Krisimasi vizuri,” alisema Pallangyo.

“Mara baada ya Mary kupika chai aliendelea na shughuli za kawaida mpaka mauti yalipomfika kwa kupigwa na shoka chumbani kwake,” alisema.

Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro alifika eneo la tukio na kusema vyombo vya usalama vimeanza msako mkali kumtafuta mtuhumiwa .

Murro aliwataka wananchi kuwa watulivu na kuviachia vyombo vya usalama kufanya kazi yake na kuwataka wananchi wenye kujua taarifa za alipokimbilia wasaidiane na vyombo vya usalama.

Katika tukio jingine, mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia jana wilayani Serengeti mkoani Mara ilisababisha vifo vya watu watatu wakiwamo watoto wawili wa familia moja na kuharibu miundombinu.

Watoto hao ni wa Hagai Kongoye mwenye umri wa miaka 10 na mwingine minne. Walifariki baada ya maji kuingia ndani wakiwa wamelala kisha ukuta wa nyumba kuanguka na kusababisha kifo chao huku mmoja akijeruhiwa.

Pia, dereva bodaboda aliyejaribu kuvuka daraja la Nyiberekera alisombwa na maji na mwili wake ulipatikana baadaye eneo hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz