Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wake ulikutwa umetupwa kituo cha ITV Mwenge

Screenshot 2021 03 28 At 08.05.04 660x400.png Mwili wake ulikutwa umetupwa kituo cha ITV Mwenge

Sun, 28 Mar 2021 Chanzo: millardayo.com

Kituo cha Television cha ITV kimeripoti taarifa za uthibitisho kuhusu kupatikana kwa mwili wa Mwandishi wake wa Habari Blandina Sembu ukiwa umetupwa njia panda ya ITV, Mwenge Dar es salaam.

Taarifa hiyo imesema Jeshi la Polisi Kinondoni limethibitisha kutupwa kwa mwili wa Mwandishi wa habari ITV/Radio one na Mtayarishaji wa kipindi cha Jarida la Wanawake Blandina Sembu katika eneo la njia panda ya ITV.

Hadi sasa Watu waliofanya tukio hilo hawajajulikana lakini imeelezwa gari walilokua wakitumia ni Noah, Polisi wanaendelea kuwasaka. #RIPBlandina Poleni nyingi kwa Familia, Ndugu, Marafiki na wenzetu wa ITV.

ULIPITWA? TAZAMA HAPA RAIS SAMIA SULUHU AKIPOKEA RIPOTI YA CAG NA KUZUNGUMZA

Chanzo: millardayo.com