Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa mtangazaji Isaac Gamba wa DW kufanyiwa uchunguzi

23022 Gamba+pic TanzaniaWeb

Sat, 20 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwili wa mtangazaji nguli wa Kitanzania aliyekuwa akifanya kazi katika Kituo cha Redio cha Sauti ya Ujerumani, Idhaa ya Kiswahili (DW), Isaac Gamba unachunguzwa na polisi na madaktari kubaini chanzo cha kifo chake.

Gamba alikutwa amefariki nyumbani kwake baada ya kutoonekana kazini siku ya Jumanne Oktoba 16 na Jumatano Oktoba 17 na wala hakutoa taarifa kama ana tatizo lolote.

Hali hiyo iliwashtua wafanyakazi wenzake, na kuwafanya waamue kwenda kutoa taarifa polisi ambao walifika nyumbani kwake na kuvunja mlango uliokuwa umefungwa na kumkuta amefariki dunia.

Baadhi ya wafanyakazi wenzake waieleza MCL Digital  kuwa hadi leo saa 6:30 mchana polisi hawajatoa taarifa yoyote na kwamba hadi jioni ya leo huenda wakawa wamepata taarifa zaidi.

Akiwa nchini Tanzania Gamba aliwahi kufanya kazi na vyombo mbalimbali vya habari, ikiwamo Radio Uhuru, ITV na Radio One.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz