Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwili wa askari wakutwa mtaroni karibu na kituo cha polisi

102412 Pic+askari Mwili wa askari wakutwa mtaroni karibu na kituo cha polisi

Tue, 14 Apr 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Askari wa kituo cha Polisi Kia wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, Sajenti Juma Ango anadaiwa kuuawa na watu wasiojulikana na kutupwa mtaroni karibu na mgahawa wa chakula Bora mita chache kutoka kituo cha Polisi Hai Mjini.

Mwili wa askari huyo aliyekuwa kitengo cha upelelezi kituo cha polisi Kia ulikutwa ukiwa na jeraha kubwa kisogoni na damu zikiwa zimetapakaa usoni.

Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya alisema April 14 saa mbili asubuhi watu waliokuwa wakifyeka majani kandokando ya Barabara Kuu ya Arusha Moshi ndio waliouona mwili huo na kutoa taarifa polisi.

Sabaya alibainisha kuwa mwili wa askari huyo ulikutwa ukiwa na jeraha kubwa kisogoni na kwamba alikuwa amepigwa na kitu chenye ncha kali.

“Taarifa zinasema alikuwa na askari wenzake juzi Jumapili ya Pasaka hadi saa nane usiku maeneo ya Msami Baa. “alisema Sabaya

Mmoja wa mashuhuda ambaye ni muuza magazeti eneo la tukio, Joyce Nguma alisema akiwa anaendelea na shuguli zake alisikia kelele kuwa kuna mwili upo mtaroni.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
“Nilienda nikachungulia nikaona huo mwili, kichwani akiwa ametapakaa damu, itakuwa aliuawa sehemu nyingine ndio wakaja kuutupa mwili wake hapo, kweli huu ni ukatili wa kinyama,” alisema Nguma.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salumu Hamduni alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi haujakamilika na pindi utakapokamilika taarifa kamili zitatolewa.

Chanzo: mwananchi.co.tz