Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti, wakazi wakimbia nyumba wakihofia polisi baada ya kutokea mauaji

68245 Vurugu+pic

Thu, 25 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Hofu ya operesheni ya vyombo vya dola dhidi ya watu wanaotuhumiwa kuhusika kwenye tukio la vurugu zilizosababisha vifo vya watu wanne katika Kisiwa cha Siza wilayani Ukerewe umewakumba wakazi wa eneo hilo kiasi cha baadhi yao kuyahama makazi yao.

Miongoni mwa wanaodaiwa kukimbia makazi yao na kwenda kusikojulikana ni mwenyekiti wa kitongoji cha Siza, Mwimari Kasanzia.

Kutokana na hofu hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella aliyetembelea kisiwa hicho juzi usiku aliwatoa hofu wananchi akiwataka waliokimbia makazi yao kurejea.

“Hakuna mwananchi atakayeonewa wala kuhusishwa isivyo halali kwenye tukio hili ambalo kusema ukweli limeutia doa mkoa wetu. Waliokimbia warejee kusaidia kupatikana kwa wahusika kwa kutoa taarifa ili hatua za kisheria zichukuliwe,” alisema Mongella.

Tukio la mauaji lilitokea Julai 22 katika kisiwa hicho na watu wanne akiwemo ofisa mfawidhi wa rasilimali za uvuvi Kanda ya Ukerewe, Ibrahim Nyangali walipoteza maisha baada ya kutokea vurugu kati ya maofisa wa kikosi cha kupambana na uvuvi haramu na wakazi wa kisiwa hicho ambao wengi wao ni wavuvi.

Wengine waliokufa ni pamoja na Damian Joseph (18), Malanja Malima (18) na Chrisant Christian (47).

Pia Soma

Watu wengine wawili, askari polisi mmoja na mwananchi walijeruhiwa.

 

Soma gazeti la Mwananchi la leo Alhamisi Julai 25, 2019 kwa taarifa zaidi

 

Chanzo: mwananchi.co.tz