Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti wa kijiji, wenzake mahakamani kwa madai ya kuchoma nyumba moto

72022 Pic+kijiji

Mon, 19 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Mwenyekiti wa kijiji cha Matembota kata ya Kisaka na wenzake watatu wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wilaya ya Serengeti kwa madai ya kuchoma moto nyumba nne za mkazi wa kijiji hicho.

Leo Jumatatu Agosti 19, 2019 mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile mwendesha mashtaka wa Serikali, Renatus Zakeo amesema washtakiwa hao walitenda kosa hilo Agosti 14, 2019.

Katika kesi ya jinai namba 121/2019,  Zakeo amewataja washitakiwa kuwa ni Keremi Getiro (49) ambaye ni mwenyekiti wa kijiji hicho; Gitegere Mokiri (49) Gesisi Chacha (38) na  Saroti Magesa (39).

Wanadaiwa kwa pamoja walichoma nyumba nne zilizokuwa na samani mbalimbali zenye thamani ya Sh5 milioni mali ya Ghati Sise mkazi wa kijiji hicho.

Washitakiwa wote wamekana shtaka na kurudishwa rumande hadi Agosti 30, 2019 kesi hiyo itakapotajwa tena.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz