Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti wa kijiji mbaroni rushwa ya ngono

Da96271c56d13d372883171a087ddc4a Mwenyekiti wa kijiji mbaroni rushwa ya ngono

Tue, 18 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Kiteto mkoani Manyara, imemkamata Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimana Wilson Ngolanya (63) kwa tuhuma za rushwa ya ngono.

Taarifa Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Manyara Holle Makungu, Ngolanya imeeleza kuwa, Ngolanya alikamatwa Agosti 15, mwaka huu jioni katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Naisio mjini Kibaya akiwa uchi wa mnyama, amevaa kondomu tayari kufanya uhalifu huo.

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari ilieleza kuwa, awali Takukuru ilipokea taarifa kutoka kwa mlalamikaji ambaye ni binti wa miaka 23 (jina limehifadhiwa), akimtuhumu Mwenyekiti wa Kijiji kwa kamuomba rushwa ya ngono.

“Kwa mujibu wa uchuguzi Ngolanya alikuwa akiomba rushwa ya ngono ili amsaidie mlalamikaji kuwaondoa wavamizi watatu kwenye shamba lililokuwa linamilikiwa na baba wa binti huyo wa ambaye sasa ni marehemu,”ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uchunguzi unaonesha kuwa Ngolanya anafahamu kuwa shamba hilo lilikuwa la marehemu baba wa binti huyo lakini alimtaka msichana hiyo ampe rushwa ya ngono ili kuwaondoa wavamizi katika shamba hilo.

Alisema binti huyo baada ya kuona usumbufu unazidi alitoa taarifa Takukuru na baada ya kujiridhisha na uchunguzi wa awali, makachero wa taasisi hiyo waliandaa mtego uliwezesha kukamatwa kwa mtuhumiwa katika moja ya vyumba kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni akiwa katika hali aliyokutwa nayo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Makungu ni kinyume cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007, mtu yeyote aliyekuwa katika mamlaka ya uongozi ambaye kwa kutumia mamlaka au cheo alichonacho akilazimisha sharti la rushwa ya ngono ili kumpa mtu ajira, kupandishwa cheo, kumpa haki stahiki, upendeleo au unafuu usiostahili.

Taarifa ilibsinisha kuwa, mtu huyo atakuwa ametenda kosa la rushwa ya ngono na ikithibitika atashahili adhabu ya faini isiyozidi milioni tano au kifungo kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Chanzo: habarileo.co.tz