Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwenyekiti TCCIA ashitakiwa  kwa uhujumu uchumi

2d6d508ef220ed6edf33a581f3452695.jpeg Mwenyekiti TCCIA ashitakiwa  kwa uhujumu uchumi

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mara, Boniphace Ndengo na mwenzake, Josephine Angolo wamefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la uhujumu uchumi.

Mwendesha mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Marshal Mseja aliwasomea mashitaka jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Stanley Mwakihaba.

Mseja alisema katika shauri hilo Namba 24 la mwaka 2021, shitaka la kwanza linawahusu washitakiwa wote wakidaiwa kula njama wakiwa kwenye ofisi za IMARA Saccos iliyopo Musoma mjini na kutenda kosa Oktoba 28 mwaka 2016.

Alisema shitaka la pili linamhusu mshitakiwa wa kwanza ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa IMARA Saccos. Ilidaiwa kuwa Oktoba 28 mwaka 2016 Ndengo alipokea Sh milioni 11 za Saccos hiyo na kuzitumia kwa matumizi yake.

Shitaka la tatu linamuhusu mshitakiwa wa pili anayedaiwa kuwa wakati akiwa mwenyekiti wa Saccos hiyo Oktoba 28 mwaka 2016 alimsaidia mshitakiwa wa kwanza kufanya ubadhirifu wa fedha hizo.

Washitakiwa hao walitakiwa kutojibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Wakili Julius Kirigiri anayewatetea washitakiwa hao aliomba mahakama iruhusu wawekewe dhamana.

Mseja alipinga hoja hiyo alisema licha ya sheria ya uhujumu uchumi kutokuwa na dhamana, mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo. Washitakiwa walirudishwa mahabusu hadi Novemba 16 mwaka huu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz