Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwendesha Mashtaka mikononi mwa Takukuru

E4588bf4c8b07ece1d35db1955666dc2 Mwendesha Mashtaka mikononi mwa Takukuru

Sun, 25 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Manyara inamshikilia Mwendesha Mashataka wa Serikali mkoani humo Wakili Mutalemwa Kishenyi kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh milioni tano.

Wakili Kishenyi alikamatwa na Maafisa wa Takukuru Aprili 23, akiwa amepokea kiasi hicho cha fedha kutoka kwa watuhumiwa wa makosa ya jinai.

Watuhumiwa hao wa makosa ya jinai walikamatwa hivi karibuni kufuatia upekuzi uliofanywa na vyombo vya dola ambapo walikutwa na vitu mbali mbali ikiwa ni pamoja na risasi 370.

Katika hatua nyingine, Takukuru mkoani Manyara imemtaka Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands, David Mulokozi kufika katikaofisi za Takukuru baada ya kukaidi wito aliopoewa kwa madia kuwa ana shughuli za kibiashara.

Takukuru imesema kukaidi wito huo ni kosa kisheria.

Chanzo: www.habarileo.co.tz