Dar es Salaam. Aliyekuwa raisi wa Migodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu, Deogratius Mwanyika(56) na wenzake, wametimiza siku 498 wakiwa rumande, huku upelelezi wa kesi hiyo ukiwa bado haujakamilika.
Washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Oktoba 17, 2018 wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 77/2018.
Kesi ya vigogo wa Acacia mambo ni yale yale
Mwanyika wa Acacia, mwenzake washtakiwa kwa makosa 39
Mwanyika na wenzake sita, wanakabiliwa na mashtaka 39, yakiwemo ya utakatishaji fedha na kukwepa kodi.
Leo, Ijumaa Februari 28, 2020 Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon ameieleza mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mkazi, Vick Mwaikambo kuwa kesi hiyo iliitwa Mahakama hapo kwa ajili ya kutajwa.
Pia Soma
- VIDEO: Uteuzi wa wagombea ACT- Wazalendo watangazwa
- Mahakama yazuia ndege kutoka China kuingia Kenya
- VIDEO: Askari aliyefukuzwa kazi kwa kumbaka mtoto wa askari apandishwa kizimbani
Baada ya kueleza hayo, hakimu Mwaikambo aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 13, 2020 itakapotajwa.
Washtakiwa wamerudishwa rumande kutokana na mashtaka ya kutakatisha fedha yanayowakabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.
Mwanyika atakiwa kwenda kwa DPP
Upande wa mashtaka kesi ya Mwanyika waomba msaada wa upelelezi nje ya nchi
Mahakama yakataa kubadili jina la Mwanyika