Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanaume ashindwa kutoroka jela akiwa amevaa nguo za kike, tembea yasababisha akamatwe

69937 Pic+jela

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Rio De Janeiro. Mfanyabiashara wa madawa ya kulevya amekamatwa baada ya kujaribu kutoroka gerezani akiwa amevalia nguo za kike.

Mfanya biashara huyo alivaa kinyago chenye sura ya kike, wigi pamoja na nguo za kike zilizomfanya aonekane kama binti wa miaka kumi na tisa.

Clauvino da Silva, mwenye umri wa miaka 42 alijaribu kutoroka kutoka gereza kubwa la usalama katika eneo la Magharibi mwa jiji la Rio de Janeiro Jumamosi alasiri, akiwa amevaa kama binti, lakini mpango wake huo ulikwama baada ya kushindwa kutembea kama msichana na kusababisha kukamatwa.

Alifanya mpango huo muda wa kutembelea wafungwa ambapo alibadilishana nguo na binti yake Ana Gabriere lakini kabla hajatoka nje kabisa maaskari walimshtukia kutokana na mwendo wake na muonekano kuwa vitu viwili tofauti.

Watu saba akiwemo mjamzito mmoja wanashikiliwa na polisi kwa kuhusika na tukio hilo akiwemo binti yake.

Chanzo: mwananchi.co.tz