Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanaume aliyemchoma kisu mkewe ahukumiwa kunyongwa

KunyongwaapiicBK M Mwanaume aliyemchoma kisu mkewe ahukumiwa kunyongwa

Tue, 17 Jan 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Dibron Said kunyongwa hadi kufa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuua mkewe Herieth Justine kwa kumchoma na kisu tumboni, begani na kifuani baada ya kumfumania na mwanaume mwingine.

Hukumu hiyo imetolewa leo Jumanne Januari 17, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu, Evodia Kyaruzi amesema kutokana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka wa mashahidi sita pamoja na ripoti ya kitabibu ya kifo cha marehemu hivyo inamtia hatiani kwa kosa la kuua kwa kukusudia.

Kyaruzi amesema kutokana na ushahidi uliotolewa na mjomba wa marehemu, Castoly Salum jinsi alivyoshuhudia mshtakiwa huyo akimchoma kisu mkewe hadi umauti unamkuta pamoja na ripoti ya hospitali hivyo Mahakama hiyo inamuhukumu kunyongwa hadi kufa.

Chanzo: mwanachidigital