Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanaume adaiwa kuwawekea sumu watoto wa kambo

Sumu Ikulu Mkl Mwanaume adaiwa kuwawekea sumu watoto wa kambo

Tue, 4 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyo ya kawaida mwanaume mmoja ajulikanae  kwa jina la Kichele Marwa mwenye umri wa miaka 48   mkazi wa mtaa wa Igelegele  kata ya Mahina mkoani Mwanza anadaiwa kuwawekea sumu kwenye uji watoto wake wa kambo kwa lengo la kuwauwa ili aishi vizuri na mama yao

Mama mzazi wa Watoto hao Deniza Felician amesema Mume wake huyo amekua akigombana nae mara kwa mara kuhusu Watoto hao watatu  aliomkuta nao akitaka awaondoe nyumbani hapo hadi ilipofika siku ya tukio hilo alipoamua kuweka sumu kwenye uji ili awauwe.

Baadhi ya majira wa mama huyo wamesema wamekua wakishuhudia matukio ya ugomvi  ya mara kwa mara katika famili hiyo.

Balozi wa mtaa huo ambae amekua akipokea taarifa za malalamiko kutoka kwa mama huyo amesema tayari hatua za kisheria zimechukuliwa dhidi ya Kichele Marwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live