Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamume amekamatwa kwa kukutwa na Dawa za Kulevya kwenye makalio

3216 Makalio 660x400

Wed, 14 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Leo February 14, 2018 nakusogezea stori kuhusu ishu ya dawa za kulevya ambapo Polisi nchini Ureno wamemkamata mwanamume mmoja kwenye uwanja wa ndege huko Lisbon, ambaye alikuwa amebeba kilo moja ya cocaine kwenye makalio bandia.

Vyombo vya habari nchini humo vilisema kuwa raia huyo wa Brazil aliwasili kwa ndege kutoka mji wa Belém do Pará, kaskazini mwa Brazil.

Haijulikani ni vipi polisi walifanikiwa kugundua hilo. Mwanamume mwingine ambaye anatuhumiwa kuwa angepokea dawa hizo alikamatwa kwenye kituo cha treni cha mji huo.

Wanaume hao watakabiliwa na kesi ya ulanguzi wa madawa ya kulevya. Mwezi uliopita polisi nchini Ureno na Uhispania walikamata cocaine ndani ya mananasi yaliyokuwa yamesafirishwa kutoka Amerika ya Kusini.

BAADA YA WIZARA YA AFYA KUHAMIA DODOMA, JENGO LAO WAMEPEWA WENGINE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Chanzo: millardayo.com