Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke mbaroni kwa mauaji ya mtoto wa dada yake

Mbaroni (1) Mwanamke mbaroni kwa mauaji ya mtoto wa dada yake

Tue, 12 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Mwanamke mmoja kwa tuhuma za mauaji ya Mtoto wa Mdogo wake aliyekuwa na umri wa miaka miwili (2) na miezi minne. Mtuhumiwa huyo LATIFA BAKARI (33), mkazi wa Mabibo aliachiwa mtoto huyo na mdogo wake kwa lengo la malezi na Tarehe 05/04/2022 mtuhumiwa alifanya mauaji hayo baada ya kumpiga kupita kiasi mtoto huyo.

Baada ya kubaini kuwa mtoto huyo amefariki baada ya kipigo, mtuhumiwa tarehe 06/4/22 aliuchukua mwili wa mtoto (marehemu), kuukunja, kuuweka kwenye ndoo ya plastiki kisha kuudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la River Side UBUNGO.

Baada ya majirani kutomuona mtoto huyo kama ambavyo si kawaida walitoa taarifa Polisi, Polisi ilimuhoji kwa kina mtuhumiwa akakiri mauaji hayo na kwenda kuwaonesha Polisi mwili wa mtoto huyo ulipokuwa. Mwili huo umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya mifumo ya kisheria kukamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live