Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke mbaroni akidaiwa kumuua mwanamke mwenzake kwa kumchoma visu

Thu, 20 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Rombo. Mwanamke anayetambulika kwa jina la Emma Lango’i (22), mkazi wa kijiji cha Samanga Wilayani Rombo, anadaiwa kuuawa na mwanamke mwenzake kwa kuchomwa na visu sehemu za shingoni na kifuani kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Koka Moita ameliambia Mwananchi leo Jumatano Juni 19,2019 kuwa wanamshikilia mwanamke huyo anayehusishwa na tukio hilo kwa mahojiano zaidi.

Aidha, Kamanda Moita amesema mwanamke huyo aliuawa usiku jana saa mbili usiku na mwili wake kutupwa barabarani.

“Hadi sasa jeshi la polisi tunamshikilia  mwanamke mmoja mkazi wa Samanga kwa mahojiano zaidi  ili kujua chanzo cha mauaji hayo, mwili umehifadhiwa Hospitali ya Karume wilayani hapa,” amesema Kamanda Moita.

Akizungumzia tukio hilo, Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Samanga, Elia Kiwelu amesema tukio hilo linahusishwa na wivu wa kimapenzi kati ya wanawake hao wawili  na kusema kuwa, kipindi cha nyuma marehemu alikua na ugomvi na mwanamke mwenzake kwa madai kuwa alikua akitembea na mume wake.

“Huyu mwanamke aliyekamatwa  kipindi cha nyuma alikua akimtuhumu marehemu anamchukulia mume wake na huyo ndiye aliyekamatwa kwa sababu kila mtu hapa kijijini anasema ndiye amehusika na mauaji hayo, alikuwa na ugomvi naye ,” amesema Mtendaji huyo.

Pia Soma

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz