Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke kizimbani kwa kusafirisha Kg 491 za dawa za kulevya

Mwanamke Kizimbani Kwa Kusafirisha Kg 491 Za Dawa Za Kulevya Mwanamke kizimbani kwa kusafirisha Kg 491 za dawa za kulevya

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja, Irene Dickson 39, mkazi wa Mapinduzi mkoani Shinyanga amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya aina ya Methamphetamine.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali, Yusuph Aboud imedai mshtakiwa Irene ambaye ni mfanyabiashara ametenda kosa hilo Novemba 8, 2022 huko katika eneo la Urafiki Ubungo Mkoani Dar es Salaam.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Mary Mrio imedaiwa, Sikh hiyo ya tukio, mshtakiwa alikutwa wakisafirisha dawa A kulevya aina ya Methamphetamine zenye uzito wa kilogramu 491.02.

Hata hivyo mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Desemba 28, 2022 kwa ajili ya kutajwa.

Wakati huo huo, MKAZI wa Kibugumo ,Kigamboni Hossen Pazi, amefikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu huyo kujibu shtaka la kusafirisha gramu 49.16 za dawa za kulevya aina ya Heroin.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Yusouph Aboud imedai Novemba 11 mwaka huu, huko Kibugumo, Kigamboni mshitakiwa huyo alikutwa akisafirisha dawa hizo kinyume cha sheria.

Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa kukosa wadhamini. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Desemba 28 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live