Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke atupwa jela miaka 45 kisa kuposti mtandaoni

Nourah Bint Saeed Al Qahtani Nourah bint Saeed al-Qahtani

Thu, 1 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja ambaye ni mwanaharakati nchini Saudi Arabia amehukumiwa kwenda jela miaka 45 kutokana na kuchapisha taarifa katika mitandao ya kijamii.

Mahakama ya ugaidi ilimtia hatiani Nourah bint Saeed al-Qahtani kwa kukiuka utaratibu wa umma kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Aidha, haijawekwa wazi ujumbe uliosababishwa akutwe na hatia licha ya kuwa inadaiwa amekuwa akiukosoa utawala wa Saudi Arabia. Nourah anafahamika nchini humo kutokana na tabia yake ya kuwakosoa viongozi wa Serikali.

Hilo ni tukio la pili kwa Mwanamke kuhukumiwa kutokana na mitandao ya kijamii, mwingine alihukumiwa miaka 34 jela mnamo Agosti 9, mwaka huu kwa kutokana na alichokuwa akichapisha kwenye ukurasa wa Twitter.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live