Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke anyongwa Geita, RPC athibitisha

Mwaibambe 4 Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Henry Mwaibambe amethibitisha tukio hilo.

Wed, 2 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linachunguza mauaji ya Mwanamke mmoja aitwaye Angela Anteli (43) Mkazi wa Mtaa wa Majengo mjini Geita aliyekutwa amenyongwa nyumbani kwake .

RPC wa Geita, Henry Mwaibambe amesema aliyefariki alikuwa ni Mama wa nyumbani katika Mtaa uliopo Kata ya Kanyara, Tarafa ya Kasamwa, Geita ambapo alikutwa amenyongwa wakati Mumewe akiwa kazini.

“Mume na Mkewe (Marehemu) wanaishi na Mtoto wa miezi sita, Mwanaume anafanya kazi kwenye Mgodi wa Dhahabu wa Geita hapa Geita, nyumba yao ile imezungushiwa na uzio, tuligundua tukio hilo kwasababu Mume wa huyu Marehemu alimtuma Kijana kupeleka maziwa nyumbani mchana, Kijana aligonga sana ile nyumba lakini haikufunguliwa"

"Nyumba ilipofunguliwa kwa njia nyingine, Mwanamke huyo alikutwa jikoni akiwa amenyongwa na hadi sasa Jeshi la Polisi linaendelea kuchunguza kiini cha tukio hilo"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live