Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke amuua mfungwa kwa busu

Mfungwaz Busu Mwanamke amuua mfungwa kwa busu

Fri, 19 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamke mmoja wa Tennessee nchini Marekani, Rachel Dollard (33) ameshtakiwa kwa mauaji ya mfungwa, Joshua Brown baada ya kumpitishia dawa za kulevya kwa njia ya ‘busu zito’ wakati alipomtembelea gerezani.

Imeelezwa kuwa, tukio hilo lilitokea mnamo mwezi Februari mwaka huu ambapo wawili hao walipigana mabusu mazito mazito wakati wa mazungumzo gerezani huku Rachel akiwa amezificha dawa hizo mdomoni mwake.

Inadaiwa kuwa baada ya tukio hilo, Rachel alimhamishia mfungwa huyo madawa aliyekuwa gerezani kwa kifungo cha miaka 11 kutokana na matumizi ya dawa za kulevya, kifungo ambacho kilipaswa kumalizika mwaka 2029.

Magereza ya Tennessee hutumia nyenzo mbalimbali kuzuia kuingizwa kwa magendo katika magereza ikiwa ni pamoja na upekuzi wa mtu yeyote anayeingia kwenye kituo.

Pia, upekuzi wa gari na seli pia kwa kutumia mbwa wa kugundua dawa za kulevya lakini bado kumekuwa na visa vya wafungwa kufariki muda mfupi tu baada ya kutembelewa na wageni wao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live