Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke Aliyeuawa Arusha Alipigwa Jembe Kichwani

Arusha MAUAJI Mwanamke Aliyeuawa Arusha Alipigwa Jembe Kichwani

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKAZI wa Njiro jijini Arusha, Jenerose Dewasi (66) amebainika ameuawa baada ya kupigwa na jembe kichwani. Akizungumza na Mwananchi msibani leo Alhamisi Desemba 30, 2021 ndugu wa marehemu, Cecy Ndosi amesema ndugu yake alikutwa na jeraha huku damu zikiwa zimesambaa sebuleni.

Ndosi ambaye marehemu ni mama yake mkubwa amesema mwili wa marehemu ulikutwa sebuleni baada ya mtoto wake Martin kuvunja mlango kutokana kuona mwili kupitia dirishani ukiwa chini ukivuja damu.

"Jembe ambalo limetumika tayari limeonekana likiwa na damu na marehemu atazikwa kesho" amesema. Amesema mtuhumiwa wa mauaji hayo ni mfanyakazi wa ndani ambaye alimchukuwa kanisani na ametoweka na kwamba chanzo cha mauaji hakijulikani.

Tukio hili limetokea siku chache baada ya mwanamke mwingine,Ruth Mmasi kubainika kuuawa eneo la Njiro pia na anayetuhumiwa ni mtoto wake wa kiume Patrick Mmasi(19).

Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Justine Masejo amethibitisha kutokea mauaji hayo kueleza yaligundulika juzi saa 2:30 asubuhi na kueleza kuwa polisi wanamsaka mfanyakazi wa ndani ambaye alitoroka muda mfupi kabla ya kubainika mauaji hayo.

Kamanda Masejo amesema mwanamke huyo ambaye alikuwa anaishi na mfanyakazi huyo kwenye nyumba yake eneo la block D mwili wake umepigwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso kushoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live