Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanamke Alewesha Wanaume na Kuwaibia

Tapeliii Mwanamke Alewesha Wanaume na Kuwaibia

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

JESHI la Polisi nchini Kenya wanamshikilia mwanamama Joyce Aluta wa Mombasa kwa kosa la kuwawekea wanaume dawa za kulevya kwenye pombe na kisha kuwaibia vitu mbalimbali kama simu, saa, viatu, wallet na pesa.

Joyce mwenyeji wa eneo la Kisimani, Nyali anadaiwa wakati mwingine kujifanya kahaba na kisha akiondoka na mteja mpaka nyumbani kwake huondoka na TV, Radio, Computer na vitu vingine.

Polisi wanamshikilia Joyce na wamefanikiwa kupata baadhi ya vitu alivyowaibia wanaume hao simu, viatu na fedha taslimu na sasa anasubiri uchunguzi ukamilike ili apandishwe kizimbani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live