Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanakwaya aliyeuawa kwa shoka Arusha azikwa

90679 Pic+shoka Mwanakwaya aliyeuawa kwa shoka Arusha azikwa

Fri, 3 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mwanakwaya Mary Richard (29) ambaye alifariki dunia kwa kukatwa shoka na mumewe, jana alizikwa na mamia ya watu, katika makaburi ya familia ya mumewe.

Makaburi hayo yapo kijiji cha Kilinga wilayani Arumeru na mazishi yaliongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Jerry Muro.

Mumewe, Moses Pallagyo ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili, anatuhumiwa kumuua mwanakwaya huyo Desemba 25 mwaka jana kwa kumkata na shoka kwa kile ambacho kimedaiwa kuwa na wivu wa mapenzi.

Inadaiwa Pallangyo aliingiwa na shetani.

Akizungumza katika msiba huo, Muro alizitaka familia hizo mbili-- ya Pallangyo na ya Mushi-- kuendeleza umoja na upendo na kwamba msiba huo usiwatenganishe na kuwa maadui.

Muro alisema vyombo vya sheria vinaendelea kushughulikia suala hilo na kuzitaka familia kuamini haki itatendeka.

Naye mtoto aliyeachwa na Mary, Raura Moses aliitaka familia ya Pallangyo kujitahidi kumsomesha mtoto huyo kwa kuwa amempoteza mama yake.

Danford Kitundu, kiongozi wa waimbaji kwaya ya Arumeru ambaye alizungumza kwa niaba ya wenzake, alisema msiba wa Mary umewasikitisha na ameacha pengo katika shughuli za uinjilisti zinazofanywa na kwaya hiyo.

Kitundu aliwataka waimbaji wenzake kumuachia Mungu na vyombo vya dola mambo yaliyotokea kwa kuwa “kazi ya Mungu haina makosa” na kila binadamu ana umri mfupi wa kuishi duniani.

Akiongoza ibada katika mazishi ya mwanakwaya huyo, mchungaji wa Kanisa na Baptist la Kiuta Songoro wilayani Arumeru, Lazaro Nnko alizitaka familia zilizokumbwa na mauaji hayo kusahau yaliyopita.

“Tujifunze kusamehe, Mungu anataka tusameheane kwa kila jambo, hivyo msiba huu uziunganishe familia mbili za pallangyo na Mushi,” alisema.

Katika hatua nyingine, viongozi wa dini kwa kushirikiana na viongozi wa mila wanatarajia kuendesha maombi maalum ya familia ya Pallangyo ili kusitokee tena mauaji mengine.

Mchungaji Nnko alisema maombi hayo yafatanyika Jumamosi saa 4:00 asubuhi nyumbani kwa familia hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz