Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanajeshi mbaroni kwa kumkata kichwa raia

Congo 867x487.jpeg Mwanajeshi mbaroni kwa kumkata kichwa raia

Wed, 12 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanajeshi mmoja wa FARDC (Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo) anayeshutumiwa kumkata kichwa kijana mmoja katika mkoa wa Kivu Kusini nchini humo, amekamatwa na atafikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi, kulingana na chanzo kutoka jeshi la FARDC siku ya Jumanne.

Sababu za uhalifu huo hazijajulikana lakini, kwa mujibu wa chanzo hicho, askari huyo amekatawa karibu na Rutshuru, kilomita 70 kutoka mji wa Mashariki wa Goma nchini DRC akiwa amelewa.

Siku ya Jumapili alasiri, "kijana mwenye umri wa miaka 16 ambaye alikuwa akichunga ng'ombe wa babake karibu na makao makuu ya Kikosi cha 12 huko Minembwe, katika eneo la Fizi, aliuawa na mwanajeshi mmoja kwa kutumia panga," Gady Mukiza, meya wa wilaya ya vijijini ya Minembwe, ameliambia shirika la habari la AFP.

“Mhanga ni mwanafunzi wa darasa la 8,” amesema. “Kichwa chake kilikatwa na askari huyu” ambaye kwa mujibu wa Bw.Mukiza alimkatakata sehemu nyingine za mwili, mkono, mguu na sehemu yake ya siri.

Jumatatu huko Minembwe, wanafunzi waliandamana "kukemea tabia ya kishenzi ya askari huyu ambaye alitakiwa kutoa ulinzi kwa raia", aliongeza meya, akibainisha kwamba mazishi ya mwathiriwa yamefanyika Jumanne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live