Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanajeshi amfyatulia risasi bodaboda aliyembeba binti yake usiku

RISASI 2222222222 Mwanajeshi mbaroni kwa kumfyatulia risasi bodaboda aliyembeba binti yake usiku

Tue, 19 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daktari wa jeshi anashikiliwa katika kituo kimoja cha jeshi jijini Nairobi baada ya kudaiwa kumfyatulia risasi dereva bodaboda aliyekuwa amembeba binti yake mwenye umri wa miaka 21 majira ya usiku.

Kitengo cha Uchunguzi wa Makosa ya Jinai kimeripoti kwamba, Wycliffe Atendo alinusurika kifo baada ya baba huyo kudhamiria kumshambulia kwa risasi.

Inadaiwa kuwa daktari huyo wa kijeshi huenda alimshuku Atendo kuwa ana uhusiano wa kimapenzi wa binti yake.

Derav huyo anadaiwa alimchukua mwanadada huyo nje ya duka moja la dawa katika Mtaa wa Kimathi, Nairobi na kumpeleka nyumbani kwao katika eneo la Syokimau, kaunti ya Machakos ambako ni safari ya takriban kilomita 20.

Wakati mwanadada huyo alipokuwa anamlipa mhudumu huyo wa bodaboda, baba'ke alitokea huku akiwa amejawa na hasira na kumpiga vibaya kabla ya kumwamrisha aingie ndani.

"Dereva huyo alipokuwa akitafakari hatua ya kuchukua, mjeda huyo mwenye hasira alitoa bunduki yake na kumfyatulia risasi. Kijana alitimka mbio kutoka eneo la tukio ili kuokoa maisha yake," Kitengo cha DCI kimesema kupitia taarifa yake.

Baada ya tukio hilo la kushtua, mwendesha bodaboda huyo alipitoa ripoti katika kituo cha Polisi cha Syokimau ambapo polisi walifika nyumbani kwa mshukiwa ili kuthibitisha madai hayo.

Dakatari huyo wa kijeshi alitiwa pingu na kuchukuliwa pampjoa bastola yenye risasi 42. Mshukiwa alipelekwa hadi kituo cha kijeshi ambapo anazuiliwa huku akingoja kuadhibiwa kwa kutumia sheria za kijeshi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live