Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanajeshi JWTZ ashikiliwa polisi kwa mauaji ya mkewe

13cd530ec6ff3c9a0f1b9092f041580c Mwanajeshi JWTZ ashikiliwa polisi kwa mauaji ya mkewe

Sat, 5 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Daniel Warioba (43) kwa tuhuma za kumwua mke wake kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Wankyo Nyigea alisema kuwa mtuhumia alimchoma mkewe kwa kutumia kitu chenye ncha kali.

Nyigesa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba 4 mwaka huu majira saa 10 alfajiri eneo la Janga wilaya ya kipolisi Mlandizi.

“Mtuhumiwa alimuua mkewe Joyce Ismail (35) ambaye ni mwaliumu wa shule ya Msingi Ruvu Darajani kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake kisha na yeye kusadikiwa kunywa sumu akitaka kujiua bila ya mafanikio,”aliema Nyigesa.

Alisema kuwa chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa na mtuhumia anashikilia ambapo amelazwa kwenye hopitali ya rufaa ya mkoa ya Tumbi kwa matibabu zaidi chini ya ulinzi.

Kwenye tukio la lingine jeshi hilo linamtafuta kijana wa shamabani (Shamba Boy) ka tuhuma za kumuua mwajiri wake Halima Pwipwi (50) kwa kumkata kwa mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Desemba, 2020 majira ya saa 3 usiku katika kijiji cha Mpaji wilaya ya Kipolisi Chalinze ambapo alikimbia mara baada ya tukio hilo.

Nyigesa alisema kuwa kijana huyo ambaye jina halikuweza kufahamika alifanya mauaji hayo ambayo hata hivyo chanzo chake bado hakijfahamika na polisi wanaendelea na msako kumtafuta kijana huyo ili hatua za kisheria zichukulie dhidi yake.

Wakati huo huo huo jeshi hilo linawatafuta watu wanaotuhumiwa kuchoma moto nyumba ya mwalimu wa shule ya sekondari Matwipili Issa Mwakilasi (40) na kusmababishia maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake,

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 30, 2020 majira ya saa 6 usiku huko Matipwili Mkange wilaya ya Kipolii Chalinze ambapo thamani ya mali zilizoungua ni Sh 235,000.

“Mwalimu baada ya kuona moto unaaka kwenye nyumba anayoihi ambayo ni mali ya shule aliona moto huo kupitia dirishani na kuanza jitihada za kuuzima moto huo na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili ake,”aliema Nyigesa.

Aliongeza kua jeshi hilo bado linaendelea kuwatafuta wahusika lakini haikuweza kufahamika chanzo cha watu hao kuchoma nyumba hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz