Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi wa bweni akutwa mtupu nyumbani kwa mwalimu

F9377a1c6b04d9574a6d88169510f80c Mwanafunzi wa bweni akutwa mtupu nyumbani kwa mwalimu

Wed, 2 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe linamshikilia mwalimu wa shule ya sekondari ya Vwawa wilayani Mbozi, Paschal Vahaye(35) kwa tuhuma za kukutwa na mwafunzi wa kike wa bweni nyumbani kwake nyakati za usiku kwa nia ya kutaka kufanya mapenzi.

Mwalimu huyo alikamatwa akiwa na mwanafunzi huyo wa kidato cha sita (jina limehifadhiwa) baada ya uongozi wa shule hiyo kuweka mtego kutokana na tuhuma za kuwapo kwa baadhi ya walimu katika shule kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wao.

Tukio hilo lilitokea Novemba 28 mwaka huu nyumbani kwa mwalimu huyo mtaa wa Ilolo, Mjini Vwawa, majira ya saa 4:30 usiku.

Mwanafunzi huyo alikutwa chumbani akiwa mtupu.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando, alithibitisha kushikiliwa kwa mwalimu huyo na kusema kuwa tayari jeshi hilo limefungua jalada la uchunguzi.

Alisema jeshi hilo liliwakamata mwalimu na mwanafunzi huyo kwa kushirikiana na uongozi wa serikali ya mtaa baada ya kupenyezewa taarifa na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi wanahusika na idara ya elimu.

"Kimsingi tuliwakamata wote, lakini baadaye mwanafunzi tulimuachia kwa kumkabidhi kwa uongozi wa shule ili waendelee na taratibu nyingine na tulifanya hivyo ili kulinda usalama wa mwanafunzi, maana baada ya tukio hilo angeweza kuchanganyikiwa na baadaye kujidhuru."

Kamanda Kyando alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa mwanafunzi huyo amekuwa na tabia ya kwenda mara kwa mara nyumbani kwa mwalimu huyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbozi, Hanji Godigodi, alisema tukio la kukamatwa kwa mwalimu huyo ni sehemu ya mkakati wa kukomesha tatizo baada ya kupokea malalamiko mara kwa mara ya walimu kujihusisha kimapenzi na wanafunzi.

"Tumepokea malalamiko mara kwa mara lakini ilikuwa vigumu kuchukua hatua bila kuwa na uthibitisho, hivyo kwa tukio hili ni wazi tutaenda kuchukua hatua kali sana ili iwe fundisho kwa wale wote ambao wanashindwa kuheshimu sheria na taratibu".

Alisema kabla ya kukamatwa kwa mwalimu huyo tayari yeye na menejimenti walianza kuchukua hatua kwa kuleta mkuu mpya wa shule ambaye ni mwanamke kwa kuwa awali alikuwa ni mwanaume licha ya kwamba shule hiyo ni ya wasichana pekee kwa upande wa kidato cha tano na sita.

Chanzo: habarileo.co.tz