Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi mbaroni tuhuma mtandao utengenezaji gongo

PINGU KUBWA.webp JESHI la Polisi mkoani Rukwa, linawashikiria watu watatu akiwamo mwanafunzi wa darasa la sita kwa tu

Mon, 18 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanafunzi huyo nwenye umri wa miaka 19 ni wa Shule ya Msingi Katusa katika Manispaa ya Sumbawanga

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Justine Masejo, alisema kuwa watu hao wamekamatwa kufuatia operesheni maalumu iliyoongozwa na mkuu wa upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoani Rukwa, Ralph Meela pamoja na maofisa wa polisi na askari.

Kabla ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao, alisema Jeshi la Polisi lilipata taarifa kuwa kuna watu katika kitongoji cha Katusa Manispaa ya Sumbawanga wanafanya biashara haramu ya kuuza gongo, kitendo kinachosababisha mkusanyiko wa watu wanaokunywa pombe hiyo bila kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizo ya ugonjwa wa Covid-19.

Kamanda huyo alisema baada ya taarifa hizo ndipo askari polisi wakiongozwa na Meela walivamia katika eneo hilo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa katika eneo la tukio, huku baadhi yao wakiwa wanakunywa pombe hiyo, akiwamo mwanafunzi huyo.

“Baada ya kuwakamata watuhumiwa hao, polisi walibaini kuwa licha ya kutenda kosa la kuuza na kunywa pombe hiyo haramu, hawakuwa wanachukua tahadhari yoyote ya kujikinga kuambukizo ya virusi vya corona kwa kuwa walikua katika mkusanyiko…hakuna hata aliyevaa barakoa wala hakuna maji ya kunawa mikono, pia hakuna kitakasa mikono cha aina yoyote,” alisema.

Kamanda Masejo alisema watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live