Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi kidato cha pili awachanganya walimu wa kiume

98596 Msichana+pc Mwanafunzi kidato cha pili awachanganya walimu wa kiume

Tue, 10 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Musoma. Jeshi la Polisi  mkoani Mara linawashikilia walimu wawili wa shule za msingi wilayani Butiama kwa tuhuma za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi wa kidato cha pili.

Akizungumza leo Jumanne Machi 10, 2020 Kamanda wa Polisi mkoa wa Mara, Daniel Shillah amesema walimu wanadaiwa kushirikiana kumtorosha binti huyo mwenye umri wa miaka 19 aliyekuwa akisoma shule ya Sekondari Kukirango.

Amewataja walimu hao kuwa ni Kelvin Mwita (32) ambaye ni mwalimu wa shule ya Msingi Kiabakari A anayedaiwa kuwa na uhusiano na mwanafunzi huyo tangu akiwa shule ya msingi.

Amesema mwalimu mwingine ni Robert Msoke (28)  wa shule ya Msingi Pida anayedaiwa kuishi na mwanafunzi huyo nyumbani kwake baada ya kumtorosha kwao akishirikiana na Mwita.

Amesema baada ya kufanya uchunguzi  wa awali wamebaini kuwa Mwita alikuwa na uhusiano na binti huyo tangu akiwa anasoma shule ya msingi, waliendelea baada ya kuhitimu elimu ya msingi.

“Tumegundua huyo Msoke alikuwa na uhusiano na huyu mwanafunzi muda mrefu na  uongozi wa kata ya Kukirango uliwahi kumuita na kumkanya juu ya tabia hiyo lakini naona alikaidi na kuendelea," amesema Shilla.

Pia Soma

Advertisement
Amesema kabla walimu hao kukamatwa binti huyo alitoweka nyumbani kwao Februari  26, 2020 na wazazi wake kutoa taarifa polisi na msako kuanza.

Amesema polisi wanaendelea na upelelezi, utakapokamilika  hatua za kisheria zitachukuliwa.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz