Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi kesi ya kina Mbowe adai polisi walimpora fedha, kumlazimisha kuimba

92980 Pic+mbowe Mwanafunzi kesi ya kina Mbowe adai polisi walimpora fedha, kumlazimisha kuimba

Fri, 24 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Lumola Kahumbi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi polisi walivyochukua fedha zake na kumlazimisha kuimba wimbo wenye maneno Dola si lelemama.

Lumola, shahidi wa 13 katika kesi ya hiyo ya jinai namba 112/2018 inayowakabili viongozi tisa wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ameeleza hayo leo Ijumaa Januari 24, 2020 wakati akitoa ushahidi mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba.

Soma zaidi: Mbowe, vigogo Chadema kuanza kujitetea Septemba 17

Kwa pamoja washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 13 yakiwemo ya uchochezi wanayodaiwa kuyatenda Februari 16, 2018 katika viwanja vya Buibui Mwananyamala.

Katika kesi hiyo mawakili wa upande wa utetezi ni Peter Kibatala, Profesa Abdallah Safari na upande wa mashtaka wanaongozwa na wakili wa serikali mkuu, Faraja Nchimbi.

Akiongozwa na Kibatala, shahidi huyo amesema katika kituo cha daladala cha Kinondoni Studio wakati akielekea kwa shangazi yake, polisi waliwakamata watu kadhaa na kuwapeleka kituo cha polisi cha Oysterbay.

Pia Soma

Advertisement

Soma zaidi: Matukio matano yatikisa kesi ya Mbowe, vigogo Chadema

Amesema akiwa kituoni hapo, waliulizwa kama wanataka kwenda msalani na wakati anakwenda polisi wawili walimsindikiza na mmoja alimtaka ajiongeze.

Amebainisha kuwa askari mmoja alimsachi mfukoni na kuchukua Sh12,700 huku akimtaka aondoke bila kugeuka nyuma. Amesema alibaki na Sh200 mfukoni na alilazimika

kutembea kwa miguu kutoka kituoni hapo hadi zilipo hosteli za chuo hicho, umbali wa takribani kilomita 10.

Kahumbi amesema walipokuwa katika kituo hicho cha polisi Osterbay askari waliwapiga kwa kutumia mikanda.

Amesema askari mwingine alimpa ngoma mmoja kati ya waliokamatwa na kumtaka apige ngoma, kuwalazimisha waimbe wimbo wenye maneno Dola si lelemama.

Soma zaidi: VIDEO: Mashinji akwamisha kesi ya vigogo Chadema

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika; naibu katibu mkuu-Zanzibar, Salum Mwalimu na Dk Vicent Mashinji.

Wengine ni wabunge Ester Bulaya (Bunda); Halima Mdee (Kawe), Esther Matiko(Tarime Mjini; John Heche (Tarime Vijijini) na Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini).

Soma Zaidi: Heche akwamisha kesi ya vigogo Chadema

Mashtaka yao ni kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018.

Kesi hiyo bado inaendelea.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Chanzo: mwananchi.co.tz