Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi chuo kikuu Tanzania mbaroni tuhuma za rushwa

91081 Pic+rushwa Mwanafunzi chuo kikuu Tanzania mbaroni tuhuma za rushwa

Wed, 8 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) nchini Tanzania  itamfikisha mahakamani mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John cha Dodoma, James Kwangulija (27) akikabiliwa na kosa la kujaribu kutoa rushwa ya Sh900,000.

Mwanafunzi huyo anatuhumiwa kutoa rushwa kwa ofisa mtihani wa chuo hicho ili asaidie kuongeza ufaulu (GPA) wa wanafunzi wenzake sita.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Dodoma, Sosthens Kibwengo amesema mtuhumiwa huyo9 atafikishwa mahakamani leo Jumanne Januari 7, 2020.

Amesema mwanafunzi huyo amefanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 15 (1)b cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa sura ya 329 marejeo ya 2018.

Amesema mwanafunzi anasoma shahada ya ualimu ya sanaa mwaka wa tatu.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kitakachojiri mahakamani

Chanzo: mwananchi.co.tz