Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mwanafunzi awachoma kisu walimu waliotaka kumchapa

Mtanzanianews 138339887 2839376046316125 2987655845833401020 N 660x400 Mwanafunzi awachoma kisu walimu waliotaka kumchapa

Wed, 13 Jan 2021 Chanzo: millardayo.com

Polisi katika kaunti ya Kisii nchini Kenya wanachunguza kisa cha mwanafunzi wa kidato cha tatu anayedaiwa kuwachoma kisu walimu wawili waliomuagiza kufika ofisi ya walimu ili kuwadhibiwa kwa kuchelewa.

Edwin Mokaya, mwalimu wa shule ya Upili ya Kisii anaripotiwa kupata majeraha mabaya katika paji lake la uso wakati mwanafunzi huyo ambaye hakutaka kuadhibiwa alipomshambulia kwa kisu.

Mwalimu wa pili naye, Elvis Maoto, ameripotiwa kupata majeraha mkononi mwake alipojaribu kumzuia mwanafunzi huyo kumshambulia Mokaya.

Wawili hao walikimbizwa katika hospitali ya Ram kaunti ya Kisii wanakopatiwa matibabu, baada ya kutekeleza kisa hicho, mwanafunzi huyo anasemekana alitoweka na kuingia mafichoni ambapo anasakwa,

Chanzo: millardayo.com